WAZIRI Kivuli wa Nishati, Jesca Kishoa amemshauri Spika wa Bunge, Job Ndugai kumuita mbele ya Kamati ya Bunge na Maadili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa madai ya kulidanganya Bunge na kushindwa kufanyia kazi taarifa za Ufisadi unaendelea katika mikataba ya kampuni ya kuzalisha Umeme wa Gesi ya SONGAS badala ya kumuita Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG Profesa Assad kwa kusema maneno ya ukweli.
Kishoa ambaye ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini ( NCCR–Mageuzi ), ametoa Rai hiyo leo jijini Dodoma ambapo amesema ufisadi huo unaendelea na umebainishwa katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2009 na ya mwaka 2018 ambapo Mwanasheria Mkuu waSerikali aliahidi mbele ya Bunge kua atalifanyia kazi ambapo mpaka sasa hajalifanyia kazi huku Bunge likishindwa kumuwajibisha.
Katika Ripoti hizo za CAG zilionyesha Tanzania mepoteza zaidi ya shilingi Trilion 1.3 na mikataba hiyo ikiendelea itapoteza zaidi hivyo Waziri huyo Kivuli pia ameomba Rais Magufuli kutumia Mahakama za Kimataifa katika swala hilo kama kwake limekua gumu ili kuokoa fedha za Watanzania.
Mke wa Kafulila Aibua Ufisadi wa Trillion 1.3 Sakata la Songas
0
January 14, 2019
Tags