Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma imeshindwa kufikia lengo la kukusanya mapato ya Shilingi Milioni 200.8 kwa mwezi kutokana na utendaji mbovu wa Watendaji, kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji huo na sio Katibu mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole kama inavyosemekana.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkoani Kigoma Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mwailwa Pangani amesema licha ya Manispaa hiyo kushindwa kufikia lengo hilo lakini kila mwezi mapato yamekuwa yakiongezeka na hivyo kuahidi kufikia lengo hilo hivi karibuni.
Mwailwa amesema kuwa taarifa zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari nchini, hakuhusika nazo yeye na kuomba msamaha kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kwakuhusishwa kwenye mgogoro usiohusika.
"Hizi taarifa zilizozagaa mimi sikuwa Mkurugenzi kwa wakati huo, hivyo natumia fursa hii mbele yenu waandishi wa habari kumuomba radhi Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, kwa kashfa hii aliyozushiwa na pia nakiomba chama cha mapinduzi radhi kwakuwa kimechafuliwa", amesema Mkurugenzi huyo.
Kufuatia kufanya vibaya kwa manispaa hiyo katika ukusanyaji mapato, Ofisi ya CAG imeipa manispaa hiyo hati chafu kwa miaka mitatu mfululizo.
Polepole alifanya ziara mkoani Kigoma mwezi Machi, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine alisikiliza kero za wafanyabiashara wa masoko yaliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji waliokuwa wakilalamikia kupanda kwa tozo za vizimba kutoka shilingi 15,000 hadi shilingi 50,000.
Mkurugenzi APANGUA Tuhuma za Katibu mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole Kushusha Mapato
0
January 03, 2019
Tags