Mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi Aongelea Bombardier Kupelekwa Service Canada Kwa Sh Bilion 13
0
January 14, 2019
Kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kuwa, Ndege 2 za Bombardier zitapelekwa nchini Canada kwa service itakayogharimu bilioni 13.9, Mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi, akiongea na TBC leo asubuhi, ameeleza kuwa, kwa kawaida ndege hufanyiwa service kwa masaa na kwamba service kubwa hufanyika kila baada ya ndege kukimbia kwa muda wa masaa 4,000.
Matindi alisema kuwa wakati wa kuifufua ATCL ilikuwa na Marubani 11 lakini kwa sasa ina Marubani 50, kati yao 48 wazawa na 02 wageni.
Mipango iliyopo ni kufikisha marubani 60.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, maboresho makubwa yamefanyika ya kuajiri wahandisi wapya na wa zamani na kufikisha idadi ya wahandisi 80.
Matindi alisema kuwa, wanatarajia kuanzisha program ya kuchukua wanafunzi kutoka vyuoni mmoja kwa moja na kuwafundisha na kwamba watakaoonyesha moyo wa uzalendo na maadili wataajiriwa.
JF
Tags