Mkurugenzi: Wakulima wa Korosho Wameshalipwa pesa Zao

Mkurugenzi: Wakulima wa Korosho Wameshalipwa pesa Zao
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mtwara Vijijini, Omari Kipanga, ameweka wazi kuwa zoezi la ulipaji wa pesa za korosho katika Halmashauri yake linaendelea, na kwamba kuna wengine wengi wameshalipwa.


Akizungumza na www.eatv.tv. Mh. Kipanga amesema kwamba malalamiko yanayotolewa mitandaoni hayana uthibisho, ila watu wanaendelea kulipwa pesa zao, huku zoezi la uhakiki nalo likiwa linaendelea na hakuna kilichosimama.

“Mimi sijapata malalamiko ofisini kwangu, ila zoezi la ulipaji bado linaendelea, mfano mimi kwenye Halmashuri yangu, tunafanya uhakiki na zoezi linaendelea, hakuna kitu ambacho kimesimama,

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema wanaanza kutembea shule mbali mbali kuangalia idadi ya watoto walioripoti, ndipo wajue kama kweli kuna watoto ambao hawajaripoti shule kutokana na wazazi kukosa pesa, kwa kutolipwa pesa za korosho.

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko katika mitandao ya kijamii kuwa baadhi ya wakulima wa korosho wameshindwa kuwapeleka watoto shule, kutokana na kukosa pesa kwa kutolipwa pesa zao za korosho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad