Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri Apiga Mkwala Mzito Kwa Wanaochukua Sauti yake na Kuichanganya na Rais


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri ameonesha kutopendezwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii, kumchonganisha na Rais John Pombe Magufuli.

Mwanri ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu ikisambaa kwa kipande kifupi cha video ambayo inamuonesha kiongozi huyo, na Rais Magufuli wakijibishana kwa maneno.

Mwanri amesema "wakati mwingine huwa naona wanavyotuweka pamoja na viongozi ambao nawaheshimu sana, si kitu kinachonifurahisha sana, licha ya kuunganisha kuleta kichekesho lakini mimim binafsi sifurahishwi nao." "Kuhusu wanaotumia sauti yangu kutengeneza muziki sina shida nao ila muhimu mimi matokeo yangu ipatikane kwa wananchi wa Tabora na wala sitakimbilia kwenye biashara eti wanilipe." ameongeza Mwanri.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri amekuwa maarufu kupitia mitandao ya kijamii hivi karibuni kwa kuanzisha misemo mbalimbali ikiwemo, sukuma ndani, fyekelea mbali, pamoja na Injinia soma hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad