Mnabahati, Mngegoma Tungefika Pabaya"- JPM

Mnabahati, mngegoma tungefika pabaya"- JPM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha Kampuni ya Bharti Airtel, kukubaliana na serikali katika kubadilisha mfumo wa uwekezaji wao na muundo wa uongozi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, Ikulu jijini Dar es salaama katika hafla ya utiaji saini baina ya serikali ya Tanzania na wamiliki wenza wa kampuni ya Airtel Tanzania ambapo sasa serikali inamiliki hisa asilimia 49 kutoka 40 ya awali na wawekezaji wameshuka hadi asilimia 51 kutoka 60 ya awali, ambapo amesema kuwa endapo wasingefikia makubaliano hayo yaliyokuwa na mvutano mkali, basi wangefikia pabaya.

"Niwashukuru tu uongozi wa Airtel kwa kukubali hili, maana wangekataa tungekuwa tumefikia pabaya na hili sio uongo", amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameongeza kuwa, "Makubaliano haya madeni yaliyokuwa yameingizwa katika Airtel yote yamefutika, tumeanza na Airtel mpya yenye Dira ya kutengeneza faida na hili ni gumu kwa sababu madeni iliyokuwa inadaiwa Airtel ilikuwa kwenye trilioni moja huko".

Sakata hilo liliibuliwa Disemba 2017 ambapo, Rais Magufuli alimtaka Dkt. Mpango kuchunguza  undani wa kampuni ya Airtel baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kampuni hiyo inapaswa kuwa chini ya umiliki wa Kampuni ya Simu (TTCL),  ambayo ni ya serikali. Pia Rais Magufuli alieleza wazi kuwa kuna ‘mchezo mchafu’ uliofanywa na baadhi ya watu katika suala hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad