Mshambuliaji wa Misri na klabu ya Liverpool ya England Mohamed Salah ameibuka mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kwa mwaka 2018.
Salah alimshinda mchezaji mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane" kutoka Senegal na mshambuliaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang. (Chini ni Kikosi cha Afrika).
Mohamed Salah alikabidhiwa tuzo hiyo katika sherehe iliyofanyika siku ya jana nchini Senegal, hii ikiwa ni mara yake ya pili kushinda tuzo hiyo.