Mtoto Wa Monalisa Apiga Division 1 na A ya Hesabu Matokeo Ya Form Four..Monalisa Afunguka


Mtoto wa Monalisa Sonia Otieno
Mtoto wa muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry ‘Monalisa’ na mtayarishaji wa filamu Marehemu George Otieno, Sonia Otieno amepata division katika matokeo yake ya form four.

Siku ya jana Baada ya matokeo kutoka Monalisa alishea kwenye Mitandao ya kijamii kuwa mwanaye ambaye alimaliza kidato cha nne mwaka jana amepata division 1 na hata kupata A ya hesabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa aliweka wazi Furaha ya binti yake kufaulu na kuandika maneno haya:
 Machozi yananimwagika. Nakosa cha kusema. Ahsante mwanangu. Divisio One? Na A ya Maths? Uwiiii, nakupenda mwanangu @soniamonalisa @soniamonalisa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad