Zari anaeeleza kuwa likizo ilikuwa nzuri na yenye uzito wa aina yake ila alijikuta akila takribani mara 15 kwa siku na suala la gym likawa la mara chache sana.
"Ni kama Jahannamu, unawezaje kufanya hivyo kwangu, bila kujali, ninakushukuru, na hivyo hivyo kwa familia yangu,tumetengeneza kumbukumbu nzuri," ameeleza Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Zari The Bosslady ambaye ni mzazi mwenza na msanii Diamond Platnumz, ni miongoni mwa watu Afrika Mashiriki wenye nguvu ya ushawishi kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wafuasi (followers) zaidi ya milioni 4 kwenye mtandao wa Instagram.