Watu tisa wametiwa mbaroni kuhusiana na shambulio dhidi ya hoteli ya kifahari mjini Nairobi, Kenya ambapo watu 21 waliuawa.
Washambuliaji wote watano waliyovamia hoteli ya DusitD2 na majengo yaliyokuwa karibu na hapo waliuawa, maafisa walisema huku msako wa kuwatafuta wale waliowasaidia kupanga shambulio hiloukiendelea.
Kundi la al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia lemekiri kuhusika na shambulio hili la siku ya Jumanne.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa watu wote waliokuwa hawajulikani waliko wamepatikana.
Kumekuwa na taarifa za kukinzana kuhusu mwanamke anayetuhumiwa kuwa mke wa mojawapo ya washukiwa wa shambulio hilo, anayearifiwa alikamatwa Kiambu kaskazini mwa mji mkuu wa Nairobi.
Polisi inasema haiwezi kuthibitisha au kupinga kwamba kuna aliyekamatwa.
'' Hatutaweza kuzungumzia upelelezi wakati huu, kwa mfano tukizungumza kuhusu Kerubo wale waliokuwa karibu na yeye watasikia tumetangaza kuwa tunamtafuta,tunafanya nini...watatoroka'', alisema msemaji wa polisi Charlse Owino.
Aliongeza kuwa cha msingi ni kuhakikisha kuwa wale wote waliyohusika na kupanga na kutekeleza shambulia hilo wanakamatwa.
Tunafahamu nini kuwahusu washambuliaji?
Chombo kimoja cha habari nchini Kenya kinaripoti kuwa anayetuhumiwa kuwa mke wa mmoja wa washukiwa wa shambulio hilo amekamtwa katika eneo la Kiambu, kaskazini mwa mji mkuu wa Nairobi.
Polisi pia inasema kuwa imemtambua Ali Salim Gichunge, anaefahamika kwa jina lingine kama Farouk, kupitia gari lililotumika kufanya shambulio hilo.
Msako wa Kuwatafuta Waliosaidiana Kupanga Shambulio Kenya Washika Kasi
0
January 18, 2019
Tags