Mtu Anayedaiwa Kufanana na Rais Magufuli Azua Taharuki Kituo Kikuu cha Mabasi Moshi



Hali ya taharuki imetokea leo asubuhi katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi baada ya kuonekana abiria mwenye mfanano wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Abiria huyo aliyefahamika kwa jina la Peter Pauli mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro alifika kituoni hapo majira ya saa 1:00 kwa lengo la kusafiri hata hivyo hakuwa tayari kueleza wapi anaelekea.

Clouds habari ilitaka kufahamu anapokeaje hisia za watu juu ya mfanano wake na Rais Magufuli, pauli hakupenda kuzungumzia suala hilo.

Hata hivyo Pauli alisema yupo tayari kuzungumzia changamoto ya usafiri iliyopo kwa mikoa ya kaskazini na kushauri kufufuliwa kwa reli ya Dar/Tanga ili kuondoa kero hiyo ya muda mrefu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad