Muswada wa Vyama vya Siasa: Bunge lapitisha muswada 'wenye utata', sasa wasubiri saini ya Rais Magufuli

Hatimaye Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania umepitishwa na Bunge la nchi hiyo na sasa utapelewkwa kwa Rais Magufuli ili ausaini na kuwa sheria.

Upitishwaji wa muswada huo umepitia vigingi kadhaa, ukikosolewa vikali na vyama vya siasa vya upinzani na asasi za kiraia ambao wanadai utaminya demokrasia nchini humo.

Hata hivyo wabunge wa chama tawala cha CCM ambao ni wengi Zaidi wameutetea muswada kwa kudai unaenda kusafisha siasa za vyama vingi.

Baada ya kupita bungeni muswada huo unatarajiwa kusainiwa na rais Magufuli ambaye serikali yake imekuwa ikibeba lawama za kuminya upinzani na uhuru wa kujieleza.

Kwa nini mswada wa vyama vya siasa unapingwa Tanzania?
Serikali Tanzania yaapa kuwanasa wauaji wa watoto Njombe
Pendekezo la kutotumia magari lapingwa Kenya
Waziri kivuli na mbunge wa Bunda, kupitia Chadema Esther Bulaya ameuita muswada huo kuwa ni 'uonevu mkubwa dhidi ya vyama upinzani.'

Uonevu kwa mujibu wa Bulaya unadhihiri kwa msajili wa vyama vya siasa kupewa mamlaka ya kuingilia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama akisema kutapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo kutoka ofisi ya msajili.

Uonevu mwengine kwa mujibu wa upinzani ni masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia kwa kuzuia vyama rafiki kutoka nje kushiriki.

"Ni haki yao ya msingi ya kueneza itikadi za vyama vyao bila kujali mipaka ya nchi…huu ni upungufu mkubwa kwani msajili anaweza kukataa tu kutokana na maslahi yake bila kuongozwa na sheria inayopendekezwa," amesema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad