Mahakama nchini Bangladesh imewaweka kizuizini wanaume saba akiweko kiongozi mmoja wa ngazi ya chini wa chama kinachotawala nchini humo cha Awami League, kuhusiana na tuhuma za ubakaji.
Mama wa watoto wanne anadaiwa kubakwa na kundi la wanaume kutokana na kwamba alipigia kura chama cha Upinzani cha Bangladesh Nationalist Party, katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.
Shambulio hilo lililofanyika wakati wa uchaguzi, limesababisha maandamano na hasira katika mitandao ya kijamii.
Hata hivyo wanaume hao wamekanusha madai hayo, na kiongozi huyo aliyehusika na ubakaji amefukuzwa katika chama.