Mwanamke Mmoja Anusurika Kifo Baada ya Kung'atwa na Nyoka Kwenye Makalio Akiwa Anajisaidia Chooni

Mwanamke Mmoja Anusurika Kifo Baada ya Kung'atwa na Nyoka Kwenye Makalio Akiwa Anajisaidia Chooni
Mwanamke mmoja nchini Australia "ameruka kutoka kwa kiti cha choo" baada ya kung'atwa na nyoka aina ya chatu.

''Nilihisi kama nimedungwa kisu kwenye mkalio ilikuwa uchungu sana, ghafla nilijipata nimeruka juu na kukimbilia nje nikiwa nusu uchi'' Richards aliviambia vyombo vya habari.

Bi Richards, 59, aling'atwa nyoka huyo katika nyumba ya jamaa zake mjini Brisbane mapema wiki hii.

Raisi wa Burundi afungua mashtaka dhidi ya televisheni
Ni changamoto gani zinazomsubiri rais mpya wa DR Congo?
Fahamu siri ya mashuka ya Kigoma
Mtaalamu wa kushughulikia nyoka Jasmine Zeleny, aliyemtoa nyoka huyo kutoka chooni hapo amesema ni kawaida kwa nyoka kutafuta maji chooni hasa wakati wa msimu wa joto kali.

Zeleny amesema kuwa Bi Richards ametibiwa na kupewa dawa ya maumivu,akielezea kuwa aina hiyo ya chatu haina simu.

Haki miliki ya pichaJASMINE ZELENY
Image caption
Nyoka huyo huenda alikuwa anatafuta maji asema mtaalamu wa nyoka, Jasmine Zeleny
"Njia ya nyoka huyo kutoka chooni ilizibwa wakati Helen alipokuwa akijisaidia, ndipo akamng'ata akihofia kudhuriwa," Bi Zeleny aliiambia BBC.

Chatu aina ya 'Carpet python' hupatikana sana katika pwani ya mashariki mwa Australia.

Je unayajua mataifa yaliopinga vazi la Hijab?
Huwa hana sumu lakini anapomng'ata mtu inapendekezwa adungwe sindano ya pepo punda.

Wiki za hivi karibuni Australia imekuwa ikishuhudia joto kali ambalo limevuja rekodi.

Wanyama wengi wa porini wameripotiwa kufa ikiwemo popo na samaki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad