Mwanamuziki Jide Atupiwa Madongo Kisa Usher Raymond


Komando wa Bongofleva anayeendelea kufanya vyema kwenye game, Lady Jaydee amekutana na upinzani wa nguvu baada ya kuweka wazi dhamira yake ya kumuona mwanamuziki wa kimataifa katika tamasha lake la 'Vocals Night'.


Kupitia katika mtandao wa Twitter mwanadada huyo alieleza namna ambavyo ndoto inaweza kutimia kwa Usher Raymond kutokea katika tamasha lake hilo.

"Mara paap! Usher Raymond huyu hapa #VocalsNight2019 . Nimejisemea tu . Dreams do come true thou . Haya ninangeni, nimeshajihami" - ameandika Jide.

Hata hivyo baada ya ujumbe huo Mwanamuziki huyo hakuachwa salama na wafuasi wa mtandao wa Twitter ambao walidiliki kukumbusha ahadi ya msaani wa Hip hop aliyedai kufanya kollabo na Tupac.

"Hahaha dada hizo ni ndoto za mchana kweupe hazina tofauti Na kaka yetu aliesema kashaimba wimbo na Tupac Shakur. Hivi karibuni utasikika" Mathias Wambua.

Sehemu ya majibizano kati ya Jide na mashabiki

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad