Mwinyi Zahera Amvua Unahodha, Kelvin Yondani ‘Siwezi kumuacha Mtu Kama Yule’

Mwinyi Zahera Amvua Unahodha, Kelvin Yondani ‘Siwezi kumuacha Mtu Kama Yule’
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameamua kumvua kitambaa cha unahodha beki wa timu hiyo, Kelvin Yondani ‘Vidic’ baada ya kutohudhuria mazoezini pasipo kutoa taarifa.


Zahera raia wa Congo amemkabidhi kitambaa hicho nyota wake Ibrahim Ajibu kufuatia kitendo cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na Yondani.

Beki huyo mwenye historia kubwa na Yanga kutokana na kudumu kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu, mwanzoni mwa msimu huu alitangazwa rasmi kuwa nahodha wa timu hiyo akirithi mikoba ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye pia alikuwa akiitumikia nafasi kama hiyo awapo uwanjani.

Taarifa zinasema kuwa sababu kubwa ya kuvuliwa unahodha ni kutokana na kuchelewa mazoezini pamoja na ukimya.

‘’Niliwapa siku tano za mapumziko ili siku ya sita waje mazoezini lakini yeye hakutokea, amezima simu na amegoma,’’ amesema Zahera.

Mkongo huyo mwenye misimamo ameongeza ‘’Siwezi kumuacha mtu kama yule anayepaswa kuonyesha mfano kwa wengine afanye hayo, hivyo nimeamua nimvue unahodha na kuanzia sasa nahodha ni Ibrahim Ajibu,’’

Itakumbukwa kuwa Mwinyi Zahera alimkataa kikosini mwake mlindalango wa klabu hiyo, Beno Kakolanya kutokana na matatizo kama hayo ambapo mpaka sasa hajajiunga na timu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad