Mzee Yusuph Afungukia Sakata La Kuvamiwa na Majambazi

Mzee Yusuph Afungukia Sakata La Kuvamiwa na Majambazi
Aliyekuwa nyota wa muziki wa taarab nchini Mzee Yusuph amefunguka na kueleza sakata la kuvamiwa na majambazi lililotokea siku chache zilizopita.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Mwananchi leo Jumanne Mzee Yusuf ambaye sasa ni mwalimu wa dini amesema pamoja na majambazi hao kumuumiza mkewe ila naye aliwapa kipigo kidogo.


Akisimulia tukio lilivyokuwa, amesema ilikuwa ni majira ya saa 2:30 usiku Jumatatu wakiwa sebuleni wanaangalia TV, wakasikia kishindo cha watu kikitua ndani ya uzio wakajua wamevamiwa na wahalifu.

Mimi kwa haraka nilipochungulia niliwaona wawili nje nikawafuata kupambana nao kumbe walikuwa zaidi ya saba na wawili walikuwa getini.

Huku nyuma watatu wakaingia ndani na kukutana na mke wangu huku wakimtaka awaonyeshe hela zilipo na kumtisha kwa bunduki, ingawa mke wangu haraka sana alibaini ilikuwa bunduki bandia ndipo alipoanza kupambana nao.

Amesema kwenye mapambano hayo kwa sababu walikuwa wengi walimzidi nguvu na kumpiga mateke ya tumboni yaliyopelekea kusikia kizunguzungu na kuanguka.

Baadhi yao tunawafahamu, wanaishi hapa mtaani na mara nyingi majirani wamekuwa wakiwahisi wana tabia hiyo ya wizi ambapk mbali na hilo kumjeruhi mkewe pia wamemjeruhi mtoto wake“.

Mzee Yusuph ametaja vitu vilivyoibiwa mbali na fedha kuwa ni simu na vifaa vya shule vya watoto

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad