Kiasi cha Tsh. Milioni 476 zimetumika kwenye mradi huo, hata hivyo umeonekana kuwa na kasoro mbalimbali licha ya kukamilika kwake, jambo lililomfanya Naibu Waziri kukasirishwa.
“Niwaonye watendaji wa Sekta ya Maji, hakikisheni mnawapa kazi wakandarasi wenye uwezo ambao watafanya kazi nzuri na kisha kuidai Serikali malipo yao; sio wakandarasi wajanja ambao wamekuwa wakila fedha za Serikali kiholela bila matokeo kuonekana”, alisema Aweso.
Naibu Waziri huyo aliendelea kwa kusema “Ndio maana nimefika Kagera kujionea fedha ambazo wizara inazitoa kama zinaleta matokeo na sio kuchezewa, huku kilio cha wananchi cha huduma ya
majisafi na salama kikiendelea. Jambo hilo halina nafasi kwenye Serikali ya Awamu ya Tano na Wizara ya Maji kwa sasa,”.