Nani Mkweli Kati ya Rose Ndauka na Mc Pilipili Kuhusu Kutoka Kimapenzi?


Baada ya Mc Pilipili kumvisha Pete ya uchumba mwanadada huyo pichani, baadhi ya watu mitandaoni wameibuka kumkejeli na kumdhihaki Actress huyo maarufu kuwa ameachwa mwenzie ndie kavalishwa Pete. Rose ameibuka kumpongeza Pilipili na kukana kuwahi kuwa wapenzi kwa kusema

"Hongera sana mshikaji wangu kwa kupata mwenza Mc Pilipili, kuna uvumi unaendelea na nahisi itakuwa vyema kama siku utapenda kuongea ukweli maana msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.....Ni hivi jamani haijawahi kutokea mimi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi,Na wala sijawahi kufikiria kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mc Pilipili zaidi ya mahusiano ya kikazi....Wanazego ebu niacheni kidogo mnamchanganya shemeji yenu....#Baada ya kusema hayo nawaombea Mungu awaongoze vyema kwenye ndoa yenu...#NatrendBilaSababu"

Hata hivyo, mwishoni mwa mwaka 2016 akihojiwa na Times fm Mc Pilipili alikiri kutoka na Rose Ndauka Ila actress huyo alikana kupitia insta kwa kupost screenshot ya Lily Ommy mtangazaji wa Times fm kwa kusema wapo kikazi Baada ya kutokea wote kwenye show ya comedy ya Dodoma.

Baadaye May mwaka 2017 akihojiwa na gazeti la Mtanzania, alipoulizwa ni star gani wa kike anamkubali zaidi MC Pilipili alimtaja Rose Ndauka kwa kumsifia kuwa yupo smart na ana miguu mizuri

Miezi sita baadaye yaani November 2017, akihojiwa na Globalpublishers MC Pilipili alikataa kutoka na Nandy Ila akakiri alishatoka na Rose Ndauka na Nicole Franklyn ambaye ni actress na Miss shinyanga na Miss Tanzania talent 2014. Tazama screenshot comments section

Na sasa Rose amekataa Tena na kumtaka Mc Pilipili auseme ukweli
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad