Nay wa Mitego "Sitamani mtoto wangu awe Mwanamuziki"



Msanii wa muziki Bongo, Nay wa Mitego amesema kuwa hatamani kuona watoto wake wafanye muziki.

Nay amesema kuwa ikitokea mtoto wake anafanya muziki atamuunga mkono japo hatamani hata mmoja ya watoto wake awe mwanamuziki kutokana na yale aliyoyapitia huko nyuma.

"Natamani siku kuona wanangu wakipambana na maisha yao na wanapambana wanakuwa na majina makubwa, ikitokea moja kati ya watoto wangu wanafanya muziki nitamuunga mkono japo sitamani kuona mmoja wapo anakuwa mwanamuziki na sababu ni historia yangu. Sipendi watoto wangu wawe wanamuziki may be sababu niliyoyapitia huko nyuma," amesema Nay kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad