Mwanamuziki Shilole amewataka wadada wa mjini 'wadangaji' kukoma kumfuatili mume wake ' Uchebe' kwa madai kwamba anamtunza na kumpendezesha.
Shilole amesema hayo baada ya kugundua kwamba wapo manyamera wanaonyemelea penzi la mume wake ambapo akidai kwamba zamani wakati akiwa hana kitu hawakuonekana kumfuata.
"Niliridhika na hali yako tangu mwanzo mpaka sasa una'shine' ila wadangaji msivyo na haya mnaanza kumwambia mume wangu Uchebe 'mekuwa handsome'", amesema Shilole.
Shilole na Ashraf Uchebe walifunga ndoa Desemba 7, 2017 ambapo awali msanii huyo alipondwa kwa kukubali kufunga ndoa na Uchebe huku maneno yakiwa kwamba hawaendani kiuwezo.