Ndugai Afunguka Kuhusu Tundu Lissu " Nafaamu Sana Kuwa Mtoro"

Ndugai Afunguka Kuhusu Tundu Lissu " Nafaamu Sana Kuwa Mtoro"
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa anamuhesabu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kama mtoro bungeni kwa sababu hadi sasa hajamwandikia taarifa yeye kama kiongozi wake kuhusu kuwepo nje ya nchi.

Spika Ndugai amesema inaelekea tayari Lissu ametoka hospitali lakini amekuwa kwenye mambo ya kuichafua nchi.

“Ila sasa hivi tunavyoongea ametoka hospitali yuko huko aliko. Inaelekea ameruhusiwa. Amekuwa akitumia mwanya huo kuzunguka na kuchafua sifa ya nchi yetu. Kwani nani amempa ruhusa?," amehoji Spika.

Ameendelea kwa kusema, 'Sasa nimwambie tu kwamba sisi tunamuhitaji maana mpaka sasa hajawahi kuniandikia chochote mimi kama kiongozi wake bungeni na wala daktari wake hajasema kitu. Kwa maana hiyo, mimi namuhesabu kama ni mtoro,'.

Utakumbuka Septemba 17, 2017 Tundu Lissu alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi
akitokea Bungeni Jijini Dodoma. Lissu alipatiwa matibabu ya mwanzo nchini Kenya kisha kuhamishiwa Ubelgiji ambapo yupo kwa sasa, hivi karibuni alifanya ziara nchini Uingereza na pia inaelezwa ataelekea Marekani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad