Ndugai Aitetea Kauli yake Kuhusu Malipo ya Lissu
0
January 31, 2019
Spika wa Bunge, Job Ndugai amedai kuwa alinukuliwa vibaya kuhusu malipo ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu.
Leo mapema, Spika Ndugai alinukuliwa akisema kwamba, Bunge limeshamlipa Tundu Lissu Sh250m, na kwamba hana madai yoyote anayoyadai Bunge kama jinsi anavyoeleza na kwamba kama akibisha atauleta mkeka.
Hata hivyo Spika amefafanua kwamba, "nimenukuliwa vibaya, sijamaanisha bunge limetoa fedha kugharamia matibabu ya Lissu. Nilichosema ni kwamba kati ya Milioni 250 alizolipwa Lissu, milioni 207 ni stahiki zake (ikiwemo mshahara), na milioni 43 ni michango binafsi ya wabunge kwa Lissu", amesema.
Ameongeza kuwa, "na sio kwamba bunge limechangia matibabu ya Lissu kama ilivyoripotiwa "Hata hivyo baad ya kauli hiyo, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amefafanua kwamba "Kwa utaratibu wa bunge, Mbunge anapokuwa anaumwa mshahara wake na posho zinalipwa kwake kama kawaida, Lissu sio mbunge wa kwanza kufanyiwa hivyo ndio utaratibu hata wa kazi zingine.Mzee Mkono mbunge msm vijijini ambae nae anaumwa mda mrefu analipwa mshahara so Lissu hapewi favor".
Tags