Kufuatia sakata la kuwarubuni wasichana wadogo kingono, nguli wa R&B Marekani na Duniani kote Robert Sylvester Kelly alimaarufu R Kelly.
Mkali huyo wa R&B ameendelea kupokea lawama kutoka kwa mastaa mbalimbali hasa kutoka hapo hapo Marekani na kuanza kumlaumu kwa kile kilichosemekana nguli huyo aliwahi kuwarubuni kingono wasichana wadogo miaka ya 2000’s, Ingawa bado haijachukuliwa hatua yoyote kisheria.
Licha ya kituo cha runinga cha LifeTime kimekuja na documentary maalumu iitwaayo ‘Surviving R. Kelly‘ ambayo inawaonesha wanawake wote waliowahi kunyanyaswa kingono na gwiji huyo wa R’n’B miaka ya nyuma.
Wanawake wengine waliozungumza kwenye documentary hiyo, ni waandishi na madensa wake ambao wamesema kuwa alikuwa anawavua nguo zote na kuanza kuwarekodi kwa kamera.
Licha ya tuhuma hizo kuendelea kumkumba R Kelly, tayari wameingilia kati mastaa wakubwa duniani akiwemo Shaffer Chimere Smith alimaarufu Neyo pamoja na mke wa Will Smith Jadapinkett Smith.
Neyo ameanza:- ” Hakuna namna, muziki ni muhimu sana na huo ndio ukweli lakini sio muhimu zaidi kuliko kuwalinda watoto wetu, kuwalinda watoto wetu wa kike ” baada ya kuandika hayo akamaliza “Nina mtoto” na kuweka hashtag ya #muteRkelly”
Ne-Yo, Smith wamtupia lawama R. Kelly, sakata la kuwanyanyasa mabinti kingono
0
January 07, 2019
Tags