Nitatekeleza kama walivyoniamuru'' - Jokate

Nitatekeleza kama walivyoniamuru'' - Jokate
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo amesema atatatua changamoto za wanafunzi wa shule ya msingi Kibuta, wilayani humo ambao walimueleza kuwa na uhitaji wa vifaa vya michezo.



Akiongea na wanafunzi hao leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika ukaguzi wa shule 3 zinazojengwa, walimweleza kuwa wanahitaji vifaa vya michezo, vifaa kwaajili ya bendi ya shule, pedi na feni.

''Wakati natoka kijiji cha Masaki nikapita Kijiji cha Kibuta na kukagua ujenzi wa shule 3 kati ya 10 ambazo tumeanza kuzijenga kama zao la kampeni yetu ya Tokomeza Zero Kisarawe. Wakaja wanafunzi wote wakaniambia niwaletee vifaa vya bendi, jezi na vifaa vya michezo, pedi na feni'', amesema Jokate.

Aidha amesema anafanya hivyo ili kuwafanya wanafunzi wawe huru kumweleza changamoto zao na amezipokea na kuahidi kuwa atatekeleza kama walivyomuaru kwakuwa yeye ni mtumishi wa wananchi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad