BAADA ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima kufanikiwa kupewa tunzo ya mchezaji bora kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi uliochezwa jana dhidi ya Mlandege na Waziri wa ujezi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohamed Ahmada, kiungo huyo amepewa majukumu mapya.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema ni wakati wa kusubiri namna ambavyo kiungo huyo myumbulifu atakavyofanikiwa kuisaidia timu yake ambayo kwa sasa ipo kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa ikiwa ni hatua ya makundi.
"Kwa sasa ni suala la muda tu, kwa Niyonzima kama gari tayari limewaka na amerejea kwenye ubora wake wa hali ya juu ambao wengi walikuwa wanamtabua, kazi yake kubwa na mpya itakuwa ni kuisaida timu yake kufanikiwa kutinga hata ya robo fainali," alisema.
Kikosi cha kwanza cha Simba ambacho kilikuwa Zanzibar leo kinatarajiwa kurejea kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa utakaochezwa Jumamosi dhidi ya JS Saoure ya Ageria.