Nkamia Kupingana na Rais Magufuli?
0
January 10, 2019
Wakati Mbunge wa Jimbo la Chemba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juma Nkamia akijiandaa kuzungumza na na viongozi wa chama chake ili kupata baraka juu ya kuendelea na mpango wake wa kupelekea bungeni hoja ya miaka 7 ya uongozi, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM,
Akizungumza na www.eatv.tv ndg. Polepole amesema kwamba Rais lazima ahudumu kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Tanzania iliyopo na tayari maamuzi ya Rais ni kutoongoza kwa muda zaidi ya ulioainisha kwenye katiba.
Polepole amesema kwamba suala la Nkamia kutaka kulipeleka bungeni hoja yake ni atakuwa anatumia uhuru wake wa kutoa maoni lakini uamuzi wa chama haupo tayari kubadilisha msimamo wa chama cha mapinduzi.
"Hoja ilishafutwa na ufafanuzi ulitolewa. Ndg. John Magufuli ataahudumu kwa mujibu wa sheria. Uamuzi wake upo bayana. Uamuzi wa chama hautabadilishwa. Hata Bunge linafanya kazi kwa mujibu wa katiba ya nchi. Vyama hukubaliana utaratibu kabla ya kwenda bungeni. hivyo silioni jambo hili likija bungeni kwa maana ya CCM", amesema Polepole.
Hivi karibuni, Juma Nkamia alisema kuwa 2019 ataanza upya mpango wa kuwasilisha hoja yake ya kufanyika kwa uchaguzi kila baada ya miaka 7, licha ya kubainisha kwamba atakutana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya wabunge wenzake.
Mwaka 2017, Nkamia alianzisha hoja hiyo ambapo alidai kwamba uchaguzi wa kila baada ya miaka 5 unaliingiza taifa kwenye gharama kubwa.
Hata hivyo, Januari 13, 2018 Rais Magufuli aliweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kutoka miaka 5-7 na pia hafurahishwi na mijadala hiyo, ambapo kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu wote kwa pamoja walisema kuendelea kwa mijadala ambayo Rais ameshaitolea ufafanuzi ni kumkosea heshima.
EATV
Tags