Beki Erasto Nyoni atakaa nje kwa wiki tatu akiuguza majeraha ya goti.
Nyoni aliumia wakati Simba ikiivaa KMKM katika mechi ya Kombe la Mapinduzi, jana.
Kutokana na maumivu, jana Nyoni alikimbizwa hospitali wakati mechi ikiendelea.
Awali Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema alikuwa ameona jeraha si kubwa sana ingawa ilitakiwa kufanya vipimo kwanza.
Nyoni ambaye alijiunga na Simba akitokea Azam FC amekuwa sehemu ya nguzo ya ulinzi katika kikosi cha Simba ambacho kimefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
Nyoni Kukaa Nje ya Uwanja Baada ya Kupata Majeraha Mapinduzi CUP
0
January 07, 2019
Tags