Ofisi ya TRA Kigoma Yamchefua Waziri Jafo


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amefadhaishwa kwa kukosekana kwa afisa wa TRA katika Kituo cha Kibiashara cha Pamoja ambacho lengo lake ni kurahisisha shughuli za kibiashara kwa wananchi wa Wilaya ya Kigoma kwa kupata huduma zote za uwezeshaji wa biashara katika eneo moja.

Licha ya kuwepo kwa kituo hicho kilichojengwa na kukamilika tangu miezi sita iliyopita lakini afisa kutoka TRA anakosekana licha ya ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Ujiji kufanya mawasiliano na TRA kwa miezi sita hadi sasa.

Kituo hicho ni miongoni mwa miradi kadhaa iliyo chini ya mradi wa Local Investment Climate(LIC) unao ratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Kutokana na hali hiyo waziri Jafo ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Kigoma kufanya ufuatiliaji wa haraka ndani ya siku nne ili kituo hicho kiweze kuwa na Wadau wote wa kutoa huduma na wananchi waweze kupata huduma ya kuanzisha na kuratibu biashara zao kwa haraka.

Inadaiwa kwamba TRA walishafika kituoni hapo na kuahidi kuleta Afisa mmoja lakini hadi leo bado jambo hilo halijafanyika hivyo kuleta usumbufu kwa wafanya biashara wanaohitaji huduma kutoka katika kituo hicho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad