Oliver Mtukudzi Azikwa Kwa Heshima Kubwa Kwao

Oliver Mtukudzi Azikwa Kwa Heshima Kubwa Kwao
Waombolezaji walisafiri kote nchini Zimbabwe ili kuhudhuria mazishi ya mwanamuziki maarufu nchini humo Oliver Mtukudzi siku ya Jumapili.

Siku ya Jumamosi , jeneza lake lilizungushwa katika msafara kupitia uwanja wa kitaifa katika mji mkuu wa Harare.

Baadaye jeneza hilo lilisafirishwa na ndege aina ya helikopta hadi nyumbani kwao , kaskazini mwa mji mkuu wa Harare.

Msanii huyo ametoa albamu 67 na kuunda mwenyewe muziki wa mtindo wa Afro Jazz unaojulikana kwa jina marufu 'Tuku music'.

Mtukudzi alifariki Jumatano iliopita akiwa na umri wa miaka 66. Siku ya Alhamisi rais Emmerson Mnangagwa alimtangaza kuwa shujaa wa kitaifa.

Msafara huo wa mazishi siku ya Jumamosi ulifuatiwa na tamasha la muziki kumuenzi mwenda zake
Alijipatia umaarufu wake 1970 akiwa mmojawapo wa sauti za uhuru zilizokuwa zikipigana dhidi ya wazungu walio wachache.

Wimbo wake wa 'Wasakara' 2001, ukimaanisha ''You are too Old'' ulipigwa marufuku kwa kuwa ulionekana kumlenga kiongozi wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe , ambaye aliondolewa madarakani kwa nguvu miaka 16 baadaye akiwa na umri wa miaka 93.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad