Ombi la Sugu kwa Rais Magufuli leo Bungeni


Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi 'Sugu' ameonyesha kuridhishwa na utendaji kazi wa wizara ya afya, huku akitoa ombi kwa Rais Magufuli.

Mbunge huyo ameeleza hayo wakati akiuliza swali la nyongeza kufuatia swali lake la msingi alipotaka kujua kuhusu ukamilishaji wa jengo la maabara katika hospitali ya rufaa Mbeya.

"Mnasema hatushukuru, naomba kuishukuru wizara hii kwa namna ilivyosimamia na kutengwa fedha Sh5 bilioni kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la maabara na ununuzi wa vipimo vya kisasa kama CT Scan na MRI," amesema Sugu.

Sugu  amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumpeleka Mbeya balozi mteule Dkt. Mpoki Ulisubisya ili awe Mkuu wa Mkoa huo kwa madai kuwa ni hazina nzuri ambayo kuipeleka mbali ni kuondoa rasilimali muhimu kwa taifa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad