Polisi watangaza kiama cha mashoga na wasagaji Nigeria

Polisi watangaza kiama cha mashoga na wasagaji Nigeria, watakiwa wahame nchi au watupwe jela
Afisa wa Juu wa Polisi nchini Nigeria, Bi. Dolapo Badmos amewataka watu wote wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuondoka nchini humo na kama wakikaidi agizo hilo basi watachukuliwa hatua kali za kisheria .

Kamanda huyo wa Polisi ambaye pia ni Msemaji wa Jeshi la Polisi Jijini Lagos, ameitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram kwa kusisitiza kuwa wale wote wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchi ya Nigeria sio sehemu yao ya kukaa.

“Kama unajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, Nigeria sio sehemu ya kuishi, tafuta sehemu nyingine. Tuna sheria zetu za nchi ambazo zinakataza mahusiano ya jinsia moja kwenye Clubs na Taasisi ambapo ukibainika unaweza kufungwa zaidi ya miaka 14,“ameandika Kamanda Badmos.


Kamanda Badmos amewataka wananchi nchini humo, wenye ushahidi kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja kutoa taarifa polisi .

Tayari tangazo hilo limezua gumzo nchini humo, tangu lilipochapishwa Januari 24, 20119. Kwani kuna matukio kadhaa ya kujeruhiwa kwa watalii ambao wanashukiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kwa mujibu wa Sheria ya Nigeria ya mwaka 2014, Watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 15 jela.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad