Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Kundi la WCB, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amejikuta akibubujikwa na machozi baada ya kumuongelea mama yake.
Sakata hilo lilitokea Wiki iliyopita kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha Wasafi Tv, ambapo Queen Darleen aliulizwa mtu gani ambaye angependa sana kumuona kwa mwaka 2019.
Queen Darleen aliingia kilio huku akisema ombi lake pekee kwa mwaka 2019 ni kuongea na mama yake mzazi ambaye hayupo naye kwa sasa hali iliyopelekea wasanii wenzake aliokuwa nao kuanza kumfariji.
Kumekuwa na tetesi kuwa Mama yake mzazi na Queen Darleen yupo kizuizini nchini China ambapo amekamatwa na madawa ya kulevya tangu mwaka jana Mwanzoni.
Queen Darleen wala familia yake hawajawahi kukubali tetesi hizo ambazo zimeshawahi kutengeneza headlines kwenye social media Lakini pia hakuweka wazi mama yake alipo kwa sasa.