Rais Magufuli leo amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri ambapo amemteua Angela Kairuki kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu/Uwekezaji.
Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko amekuwa waziri kamili wa madini, na Stanslaus Nyongo ataendelea kuwa maibu waziri wa wizara hiyo
Sambamba na hilo Rais Magufuli ameteua Makatibu Wakuu wanne na Naibu Makatibu Wakuu wawili, ili kujaza nafasi za Makatibu Wakuu waliostaafu kama ifuatavyo;
Joseph Nyamhanga - Katibu Mkuu TAMISEMI
Zainabu Chaula – Katibu Mkuu Afya
Elius Mwakalinga – Katibu Mkuu Ujenzi
Doroth Mwaluko – Katibu Mkuu Sera
Doroth Gwajima - Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI
Francis K Michael - Naibu Katibu Mkuu UTUMISHI
Vile vile Rais Magufuli amemteua Dkt. Mpoki Ulusubisya kuwa Balozi, ambaye kituo chake cha kufanyia kazi kitatangazwa baadaye.
Pia Rais Magufuli amefungua Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Cuba ambao utakuwa katika mji wa Havana, na Balozi wake atatangazwa hivi karibuni.
Rais Magufuli Afanya Mabadiliko Baraza la Mawaziri....Afungua Ubalozi Mpya Nchini Cuba
0
January 08, 2019
Tags