Rais Magufuli Afunguka Mazito Sakata la Dhahabu ya Mamilioni ya Pesa Iliyonaswa Mwanza

Rais Magufuli Afunguka Mazito Sakata la Dhahabu ya Mamilioni ya Pesa Iliyonaswa Mwanza
Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania-IGP Simon Sirro  kwa kuhakikisha watuhumiwa wote wa Dhahabu ya mamilioni ya pesa iliyokuwa inatoroshwa jijini Mwanza wamekamatwa wakiwemo Askari polisi 8.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo Leo Jumatano January 9, 2019  Ikulu Dar es Salaam wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua jana.

Akisimulia kwa kina kuhusu tukio hilo, Rais Magufuli amesema watuhuhiwa hao walikamatwa January 4 Misungwi, kisha wakarudishwa kituo kikuu cha kati, lakini hawakuwekwa Mahabusu.

"Ile dhahabu, Watuhumiwa wale walishikwa tarehe 4, wakarudishwa Mjini Mwanza na Kikosi cha Polisi nane, wakawapeleka Central wala hawakuwaingiza ndani wakawa wanajadili namna ya kuwapa hela, wakawaambia watawapa Bilioni 1. "  Amesema Rais Magufuli

Amesema, watuhumiwa hao walitoa Rushwa ya milioni 700, ikawa imebaki milioni 300 ambayo polisi hao waliahidiwa kwamba watapewa wakifika Sengerema.

Rais Magufuli ameendelea kusimulia kuwa, usiku huo  watuhumiwa waliondolewa Central  huku wakisindikizwa na Polisi hao kuelekea Sengerema.

Amesema taarifa za kiintelijensia zikawa zimemfikia, akatoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwamba watu hao wafuatiliwe haraka na wakamatwe.

Rais amesema, Polisi toka Sengerema waliweka kizuizi na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao pamoja na Polisi waliokuwa wakiwasindikiza. Polisi hao walinyang'anywa silaha zao, wakapigwa pingu na wako mahabusu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad