Amesema hayo katika Utiaji saini mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
'Ninafurahi hata ununuzi wa Korosho unaenda vizuri, ninajua wanao piga kelele sasa hivi ni wale wanaoitwa Makangomba kwasababu walinunua Korosho walifikiri watalipwa hela, wanapoulizwa mashamba yako wapi hawayaonyeshi," amesema Rais Magufuli.
Utakumbuka November 12, 2018 Rais Magufuli alitangaza uamuzi wa serikali wa kununua korosho zote za wakulima msimu huu kwa bei ya Tsh. 3,300 kwa kilo baada ya wanunuzi binafsi kushindwa kutimiza maaangizo ya serikali kwa kuanza kununua kwa kususua na kwa bei isiyoridhisha.