Rais Magufuli Kafuata Nyayo za Muamar Gaddafi


Ukitaja jina la Muamar Gaddafi, Afrika nzima inamjua ni jinsi gani alikuwa kiongozi shupavu kwa nchi yake ya Libya, mzalendo na mwenye mapenzi makubwa kwenye bara la Afrika.


Hili utakubaliana na mimi, kama wewe ni mfuatiliaji wa Historia ya Afrika na viongozi wake, kamwe huwezi kutenganisha upendo wa Gaddafi kwa Afrika, licha ya kasoro ambazo alikuwa nazo kama kiongozi na kama binadamu.

Wakati wa uhai wake, Muamar Gadafi popote ambapo alionekana, basi kwenye bega au kifuani kwake lazima alikuwa akiweka nembo 'badge' ya bara la Afrika, iwe ya kibandiko au ambayo imedariziwa vizuri kabisa kwenye kila vazi alilovaa.

Kitu hiki pia tunakikuta kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, licha ya kuvaa suti zake mbalimbali, lakini hasahau kuambatanisha nembo hiyo inayoonesha mapenzi makubwa kwa waafrika. Kila anapokuwa na shughuli ya Kitaifa, akihutubia umma, au kila anapokuwa na 'public appearance', lazima utamkuta na nembo ya bara la Afrika, aliyoiweka kifuani kwake upande wake wa kushoto.



Badge hii kwa wengine inaweza ikawa ni urembo tu, lakini kwa wenye kuelewa maana, inabeba ujumbe mkubwa sana kwa watu wenye mapenzi na bara hili, ikiwa ni pamoja na kulibeba bara la Afrika na kulitangaza popote utakapokuwa, na kufanya watu wakujue kuwa wewe ni Muafrika na unajivunia bara lako.

EATV

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad