Rais Mnangagwa Akatisha Ziara Yake ya Ulaya

Rais Mnangagwa Akatisha Ziara Yake ya UlayaRais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amekatisha ziara yake nchi za nje kufuatia kuongezeka za hasira kuhusiana na vurugu zilizosababishwa na vyombo vya ulinzi vinavyopambana na waandamanaji wanaoipinga serikali.

Rais Mnangagwa amesema kipaumbele chake cha kwanza ni kuifanya Zimbabwe kuwa na utulivu na imara.

Kiongozi huyo alipaswa kuelekea katika mji wa Davos, Uswisi kushiriki katika Jukwaa la Kiuchumi duniani, kwa lengo la kutafuta vitega uchumi kwa ajili ya nchi yake.

Maandamano hayo yamesababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kundi moja la haki za binadamu limesemna majeshi ya ulinzi toka kuanza kwa maandamano hayo yameua watu kumi na mbili na kuwakamata zaidi ya mia moja.

Mwandishi mmoja wa habari nchini humo ameiambia BBC kwamba watu wengi wamekuwa wakikamatwa kutoka katika nyumba zao na kupigwa na watu waliovalia sare.

Mkoba uliojaa madola ya Mugabe waibiwa
Jeshi 'lina hatia' ya kutumia nguvu dhidi ya upinzani Zimbabwe
Akizungumza na gazeti la serikali Msemaji wa Rais George Charamba amekilaumu chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) kwa ghasia hizo zinazotokea kwa kuunga mkono waandamanaji.

'' Kiongozi wa MDC imekuwa ikisisitiza ujumbe wake kwamba itatumia ghasia za mtaani kuyapindua matokeo ya uchaguzi wa mwaka uliopita'' alisema Charamba.

Upinzani nchini humo umepinga uamuzi wa mahakama uliotolewa mwaka jana mwezi wa Nane kuthibitisha kwamba Rais Mnangagwa amemshinda mgombea wa MDC Nelson Chamisa.

Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Zimbabwe kuacha kile ilichokiita matumizi ya nguvu yanayofanywa na jeshi kwa kinachoelezwa kuwa utafutaji wa nyumba kwa nyumba na kwa kutumia silaha za moto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad