Rais wa Gabon Ali Bongo arejea nchini mwake wiki moja baada ya jaribio la mapinduzij

Rais wa Gabon Ali Bongo arejea nchini mwake wiki moja baada ya jaribio la mapinduzi








Rais wa Gabon Ali Bongo anarejea nchini mwake leo Jumanne baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miezi miwili akipokea matibabu nchini Morocco.

Bw Bongo anarejea wiki moja tu baada ya jeshi nchini humo kufanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya serikali yake.

Kiongozi huyo mwenye miaka 59 amekuwa akipokea matibabu nchini Morocco tangu Oktoba 24 alipopata kiharisi akihudhuria mkutano mkuu wa kiuchumi nchini Saudi Arabia.

Baada ya utata kuhusu hali yake, makamu wake hatimaye alitangaza mwezi Desemba kwamba alipatwa na kiharusi.

Mara pekee kwake kuonekana na umma ilikuwa ni wakati wa hotuba ya kila mwaka ya Mkesha wa Mwaka Mpya ambayo ilirekodiwa
Serikali yazima jaribio la mapinduzi Gabon
Alieleza kwamba alikuwa amepitia "wakati mgumu."

Wakosoaji wake walitumia hali kwamba alionekana dhaifu na sauti yake kutokuwa na nguvu sana kueleza kuwa hali haikuwa shwari.

Wiki iliyopita, jeshi nchini humo lilizima jaribio la mapinduzi ya serikali na kumkamata kiongozi wa kundi hilo na pia kuwaua wanajeshi wawili waliokuwa wamevamia kituo cha redio ya taifa.

Wanajeshi hao walisema walihisi hotuba ya Bw Bongo ya Mwaka ilidhihirisha kwamba kiongozi huyo alikuwa amepoteza uwezo wake wa kuliongoza taifa hilo.

Mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu Julien Nkoghe Bekale alitangaza mabadiliko katika baraza la mawaziri.

Katiba ya Gabon inasema mawaziri ni lazima wale kiapo mbele ya rais.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad