Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema oparesheni imekamilika

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema oparesheni imekamilika
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa oparesheni ya kukabiliana na washukiwa wa ugaidi waliovamia hoteli ya Dusit2 mjini Nairobi imekamilika na kwamba washambuliaji wote ''wameangamizwa''.

Watu waliyokuwa wamejihami kwa silaha siku ya Jumanne walivamia jengo la hoteli ya kifahari ya Dusir2 katika eneo la Westlands katika jiji kuu la Nairobi nchini Kenya na kuwaua watu 14.

Awali maafisa walitangaza kuwa oparesheni hiyo ilikamilika saa kadhaa baada ya shambulio hilo lakini mlilio ya risasi na milipuko ilisikika mapema alfajiri ya leo (Jumatano)

Haijabainika ni washambuliaji wangapi walihusika na shambulio hilo.

Akihutubia taifa kwa moja kwa moja kupitia televisheni kutoka Ikulu, rais Kenyatta amesema kuwa watu 14 waliuawa katika shambulio hilo na wengine 700 kuokolewa kutoka jengo hilo.

Shirika la msalaba mwekundu hata hivyo limeripoti kuwa waliyofariki katika mkasa huo ni watu 24.

Raia wa Marekani ni miongoni mwa waliyofariki, imesema wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Washambuliaji wawili walinaswa na camera za CCTV wakiingia kwenye jengo lililoshambuliwa
"Sasa naweza kuthibitisha kuwa oparesheni ya usalama katika jengo la Dusit imekamilika mna magaidi wote wameangamizwa," alisema rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

"Tutahakikisha kila mmoja aliyehusika na shambulio hili kwa njia moja au nyingine iwe ni kupanga, kufadhili ua kutekeleza shambulio atakabiliwa vikali," ameapa kuwa serikali yake hatachelea kuwakabili vikali''.

"Hili ni taifa linaloongozwa kupitia sheria - taifa ambalo linajivunia amani upendo na umoja ... Lakini ni lazima ieleweke kuwa hatuwezi kuwaachilia huru wale wanaotudhuru sisi na watototo wetu."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad