Rais wa Zimbabwe Mnangagwa arejea nyumbani: Hali bado si shwari

Rais wa Zimbabwe Mnangagwa arejea nyumbani: Hali bado si shwari
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerejea nyumbani baada ya ziara yake nchini Urusi, kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

Serikali ya Zimbabwe imekuwa ikiulaumu upinzani kutumia hali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo, kuchochea ghasia.

Aidha upinzani umesema wanachama wake wamekuwa wakichukuliwa hatua kali kama hatua ya kujibu vurugu za maandamano yanayofanywa kupinga ongezeko la mafuta.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic ChangeNelson Chamisa amesema wengi wa wanachama wao wamekamatwa wakiwemo wabunge watano, huku afisa wake mwingine mwandamizi amejificha.

Amesema vyombo vya ulinzi vimekuwa vikikamata familia za watu majumbani mwao.

Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa watu 12 wameuawa katika ghasia hizo. Hata hivyo idadi hiyo bado haijathibitisha.

Jumuia ya Wafanyakazi iliyoitisha maandamano hayo imesema kiongozi wake Japhet Moyo amekamatwa pia.

Hapo jana Mahakama kuu mjini Harare ilitoa uamuzi kuwa waziri wa serikali hana haki ya kuagiza kufungwa kwa mawasiliano ya internet.

Huku hali ya wasiwasi ikiongezeka, serikali Jumapili ilisema kuwa hatua za vikosi vya usalama ni 'utangulizi wa mambo yanayotarajia kushuhudiwa'.

Upinzani umepinga uamuzi wa mahakama mnamo Agosti 2018 uliothibitisha ushindi wa rais Mnangagwa dhidi ya Chamisa.

Upinzani umesema nini?
Chamisa ameiambia BBC kwamba 'hakuna sababu yoyote ile ya wanajeshi kutumia silaha za moto barabarani, kuwapiga raia".

watu wanafuatwa nyumbani kwao, wanatolewa nje na familia zao hata kama wamelala... watu wengi wamekamatwa bila ya sababu ya maana," amesema.

Mwenyekiti wa kitaifa wa MDC Thabitha Khumalo amesema kwamba amejificha baada ya polisi na jeshi kuzuka nyumbani kwake usiku.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad