Rayvanny Afunguka Kuhusu Alivyojisikia Baada ya Kufungiwa Kwa Wimbo wa Nyegezi


Msanii wa Muziki Bongo, Rayvanny baada ya kufungiwa wimbo wa 'Mwanza' aliomshirikisha Diamond Platnumz amesema jambo lile lilikuwa kama funzo.

Rayvanny amesema kuwa alijisikia vibaya ila anaamini kila kitu kinatokea kwa sababu na kukitokea jambo linakuwa ni funzo.

"Nilijisikia vibaya ila naamini kila kitu kinatokea kwa sababu either kujifunza au kukumbusha jambo kwahiyo hii kwangu mimi siichukulii kama sehemu ya maumivu nachukulia kama sehemu ya darasa na kujifunza this time around mambo yako hivi hiki kitu natakiwa nifanye hiki natakiwa nisifanye," alisema Rayvanny kwenye mahojiano yake na Wasafi Tv baada ya kuhojiwa kuwa alijisikiaje baada ya kufungiwa wimbo wa Mwanza.

Ikumbukwe wiki kadhaa, Msanii huyo na Diamond Platnumz walifungiwa na Baraza la Sanaa kutojihusisha na muziki kwa muda usiojulikana kutokana na wimbo wao kutokuwa maudhui mazuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad