RC Olesendeka Agiza Watekaji Wa Watoto Wasakwa Popote Walipo

RC Olesendeka Agiza Watekaji Wa Watoto Wasakwa Popote Walipo
Mkuu wa mkoa wa Njombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Christopher Olesendeka amesema vyombo vya ulinzi na usalama vitawasaka popote walipo watekaji wa watoto watatu wa familia moja wanaodaiwa kutekwa january 20 na kusababisha taharuki kwa wakazi wa mkoa huo.

Wimbi la kutekwa kwa watoto wadogo limezidi kutanda mkoani Njombe tangu liibuke desemba mwaka jana ambapo hadi sasa inaelezwa zaidi ya watoto 10 wametekwa huku wachache wanaopatikana wanakutwa wakiwa wamefariki dunia.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikando kata ya Kichiwa wilaya Njombe ambao wamekuwa wakiwatafuta watoto wao bila kukata tamaa usiku na mchana huku wakipigwa na jua na mvua bila mafanikio , Mkuu huyo wa mkoa amesema jeshi limejipanga vyama kuwabaini wahusika wa matukio ya utekaji na mauaji na kuliagiza jeshi la polisi kupitia upya leseni za waganga wa jadi,kuwahoji na kuwafutia leseni waganga wanaojihusisha na upigaji wa ramri chonganishi kwa kuwa ndiyo wamekuwa chanzo cha matatizo hayo.

Hali hiyo ya matukio ya utekaji wa watoto ambayo yameambatana na mauaji yakihusishwa na imani za kishirikina , inakigusa chama cha mapinduzi ambapo katibu wa hamasa na chipukizi mkoawa Njombe Johnson Mgimba ambaye anakiri kuumizwa kwa kiasi kikubwa na mikasa hiyo na kueleza kuwa idara yake inaunda kikosi kazi kitakachoingia msituni kuwasaka watekaji ili kunusuru maisha ya watoto.

Izack Mwinami na Lazaro Kipagatie ambao ni wakazi wa Ikando wanaeleza jinsi walivyowatafuta usiku na mchana watoto waliotekwa bila ya mafanikio na kutoa rai kwa jeshi la polsi kuongeza nguvu ya uchunguzi wa matukio hayo.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi tayari watu wawili wanashikiriwa kwa kudaiwa kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto huku pia ikielezwa waganga ishirini wanahojiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad