Ronaldo aingia katika makubaliano na mahakama ili kukwepa kifungo jela

Ronaldo aingia katika makubaliano na mahakama ili kukwepa kifungo jela
Nyota wa soka Cristiano Ronaldo ameingia katika makubaliano na mahakama ya Madrid kuhusu madai ya kukwepa kulipa kodi baada ya kubali kupigwa faini ya €18.8m (£16.6m) fine. makubaliano yaliofikiwa yanashirikisha kifungo cha miezi 23 jela

Jaji mmoja alikataa ombi la mchezaji huyo kuhudhuria kesi hiyo kupitia kanda ya video ama hata kuingia katika jumba hilo kwa kutumia gari ili kuzuia kuandamwa na vyombo vya habari.

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 22.01.2019
Maurizio Sarri: Ni vigumu 'kuwashawishi' wachezaji wa sasa wa Chelsea
Mourinho: Nimekataa 'ofa' tatu za ukufunzi
Nchini Uhispania, wafungwa huwa hawahudumii kifungo cha chini ya miaka miwili.

Hali ya makosa ya Ronaldo inamaanisha kwamba hatohudumia kifungo jela.

Kesi hiyo ilichukua dakika chache baada ya Ronaldo kukubali makubaliano yaliotolewa na viongozi wa mashtaka

Mchezaji huyo wa Juventus ambaye aliichezea klabu hiyo usiku wa kuamkia mashtaka hayo aliwasili akiwa anatabasamu.

Wakili wake alikuwa amehoji kwamba kutokana na umaarufu wake , alipaswa kutotumia lango kuu la mahakama kutokana na hali ya usalama

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad