Rapa huyo anayefanya kazi zake chini ya Demo Production amesema kuwa anaamini kuwa umri wake bado mdogo hivyo hana papara na mapenzi.
"Mapenzi yapo, napenda familia yangu, nampenda Mwenyenzi Mungu, napenda pesa, mimi mdogo sana, am very young, yaani sio kwamba hawapo ambao hawatamani kuwa na Rosa Ree lakini hatuendani," Rosa Ree ameiambia Wasafi TV.
Kwa sasa Rosa Ree anafanya vizuri na wimbo wake unaokweenda kwa jina la Banjuka ambao uliuachia mwaka jana mwishoni.