RPC Wankyo Awatangazia Kiama Trafiki Wala Rushwa

RPC Wankyo Awatangazia Kiama Trafiki Wala Rushwa
Askari wa Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi na kuacha kuomba na kupokea rushwa.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Wankyo Nyigesa wakati akizungumza na askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Kibaha mkoa wa Pwani.

Amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya askari wa usalama barabarani kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya Jeshi la Polisi.

“Katika kipindi cha uongozi wangu nitakuwa mkali na sitosita kuchukua hatua kwa askari yeyote atakayebainika kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa madereva,”amesema Wankyo

Aidha Wankyo, amewataka askari hao kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaowahudumia kila siku na kuacha vitendo vya malumbano na majibu yasiyozingatia utu kwa wale wanaowahudumia katika barabara.

Hata hivyo, amewaasa madereva wanaoingia ndani ya mkoa wa Pwani kuzingatia sheria za usalama barabarani na wale watakaokaidi kutii sheria hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad