Sababu ya Haruna Niyonzima kufeli ndani ya Simba


Uhamisho wa mchezaji kutoka timu pinzani kwenda nyingine huwa una athari nyingi ikiwemo kutokukubalika au kuaminiwa na timu mpya hali ambayo hupelekea mchezaji husika kutopewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini kwa Niyonzima hali imekuwa tofauti.

Haruna Niyonzima alisajiliwa Simba akitokea Yanga Julai 2017 ambapo alicheza msimu wa 2017/18 lakini hakupata nafasi ya kutosha kwa walimu kama Joseph Omog, Masoud Djuma na Pierre Lechantre.

Kupitia kwa msemaji wa Simba, Haji Manara sababu ya Niyonzima kutopata nafasi ya kucheza kwa makocha hao haikuwa kutoaminiwa bali ni majeraha yaliyokuwa yanamsumbua ambayo bila shaka sasa yamekwisha na taratibu ameanza kutumika ipasavyo chini ya kocha Patrick Aussems.

Msimu huu tayari Haruna ameonekana kwenye mechi kadhaa ikiwemo ile ya Simba dhidi ya KMC ambapo alitoa pasi ya goli la Adam Salamba lakini pia jana amecheza mechi ya Mapinduzi dhidi ya Mlandege ambapo alifunga bao moja kwa njia ya penalti.

Wachezaji waliohama kutoka Simba kwenda Yanga miaka ya hivi karibuni ni Kelvin Yondani, Hassan Kessy na Ibrahim Ajibu ambao wote wamekuwa wakifanya vizuri.

Swali linabaki kuwa ni kweli Niyonzima alisumbuliwa na majeraha tangu asajiliwe Simba au walimu hawakuwa wanamwamini hatua ambayo ilipelekea mpaka kutoitwa timu ya taifa kwenye mechi za hivi karibuni kuwania kufuzu AFCON.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad