Sababu ya video ya Bilnass na Roma kutumia watoto wa MADEE na Chonge

 Roma na Bilnass wakiwa na watoto, Madee (kulia) akiwa na mwanaye Chonge


Msanii wa Hip Hop kutoka kundi la Rostam, Roma amezitaja sababu za yeye pamoja na Bilnass kuamua kuwatumia watoto wa mastaa katika video ya wimbo wa 'Funga geti'.




Video ya wimbo huo ulioachiwa wiki iliyopita imewatumia watoto wawili, mtoto wa msanii wa vichekesho, Anko Zumo aitwaye Mai Zumo pamoja na mtoto wa Madee aitwaye Chonge.

Akizungumza katika Planet Bongo ya East Africa Radio wakati wakiutambulisha wimbo huo, Roma amesema, "sababu ya kuamua kuwatumia wale watoto ni kufanya kitu cha tofauti, badala ya kutumia kila siku video vixen tukaamua kufanya vile, lakini pia Bilnass wazo lake lilikuwa ni kuwa baba na mimi pia niwe baba mwingine".

Baada ya kumtafuta Madee juu ya kumuhitaji mtoto wake, Roma amesema kuwa Madee alitaka kwanza apatiwe wimbo ausikilize na familia yake ndipo aliporuhusu na alimleta mwenyewe mtoto wake 'location'.

Pia Roma amezungumzia jinsi walivyofanya nao kazi watoto hao, ambapo amesema ilikuwa rahisi kufanya kazi na Mai Zumo kwasababu ni mkubwa kuliko Chonge, pia ni mzoefu wa kuigiza.

"Mai ni mbaya sana, yaani kila ukimwelekeza kitu anafanya hapohapo, tofauti na Chonge ambaye kwanza alikuwa na vurugu sana, alichafuka kabla hata ya 'director' kuwasha kamera, ilikuwa hata ukimkalisha mezani anachana hadi 'material' yote".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad