Serikali Yateketeza Trey 700 za Mayai Kahama

Serikali Yateketeza Trey 700 za Mayai Kahama
Serikali wilayani Kahama, imeteketeza trei 700 za mayai yanayosadikiwa ya Kuku yalioingizwa nchini kinyume cha sheria.

Agizo hilo lilitolewa na Serikali ya Wilaya ya Kahama, kupitia Ofisa Mifugo wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Dk. Damian Yustin la kuteketeza trei hizo za mayai za mfanyabiashara Regine Ayinkamiye.

Alisem mayai hayo kutoka Rwanda yalikuwa yakisafirishwa na gar T.318 AER Fuso.

Dk .Yustin alisema wafanyabiashara wanaosafirisha ama kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi wanatakiwa kufuata taratibu, ili kuepuka hasara itakayojitokeza kwa kuteketezwa kwa mali zao pindi watakapobainika kuingiza ama kusafirisha kinyume cha taratibu.

Alisema serikali imezuia uingizwaji wa mayai kutoka nchi za nje kwa lengo la kujikinga na homa ya ndege.

Alisema licha ya wafanyabiashara wa mayai kupatiwa elimu namna ya kupata vibali vya uingizwaji wa mayai na kuku ambavyo hutolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa lengo la kuwaepusha wasiendelee kupata hasara, lakini wamekuwa wakienda kinyume na kuingiza mayai na kuku kwa njia za panya.

Aidha, alitoa elimu juu ya sheria ya Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) inayosema chakula chochote kinachoingizwa nchini bila ya kuwa na kibali cha uingizwaji na usafirishaji sio salama kwa matumizi na kuongeza wafanyabiashara wataendelea kupata hasara kama watashindwa kufuata sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad