Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akipokea Madawati kutoka kwa Benki ya NMB, ndipo akakutana na changamoto hiyo ambayo imejitokeza pia katika Sekondari ya Tandahimba ambako wamejitokeza Wanafunzi wa Nne.
''Wanakisingizio flani flani hii ni dalili ya kwamba Jamii bado iko duni na tutapambana kung'oa misumari kwa winchi, hii ni dalili ya jamii duni na haijitambui kabisa chini ya Jua nawaambieni jamii isiyojitambua itakua masikini wa kudumu hata ukipata mapesa haitakusaidia kama hauna Elimu''
Alisema Waryuba
Pia amesema wanataka kupata kisingizio eti kwa sababu hawajalipwa hela za Korosho ndio kisingizio wanacholeta wakati Rais ametoa Elimu bure.